Jambo la nne;Viapo vya wakuu wa makabila na miungu yao yatosha kabisa kukuunganisha na madhabahu baali, Hii pia ni njia mojawapo ya kukuunganisha na miungu ya kigeni ukisoma Habakuki 3:9” Uta wako ukafanywa wazi kabisa; Viapo walivyopewa kabila vilikuwa neno thabiti; Ukaipasua nchi kwa mito” utaona kuwa kuna viapo

tosha kabisa juu ya kabila na vina uthabiti ju ya mfumo wako wa badae.

Angalia Amosi 1;6-8 kufungwa kwa kabila ni juu ya maaganao au viapo wa miungu yao ya kikabila ndio maana huenda maisha yako yamefungwa kwenye madhabahu ya kiakabila.

Chunguza vizuri katika Amosi 1:6-8 – Hapo unaona kabila zima limepigwa pingu na kufungwa kisha kutiwa katika mikono ya Edomu (roho ya kuhangaika na kufa vibaya) nguvu hiyo ya kulifunga kabila zima ilitoka kwenye kati ya miji ile 5 ya wakuu wa Wafilisti (wakuu wa giza) waliokuwa wanatawala miji mitano ya wafilist. Kwa hiyo kabila zima lilifungwa kwa upako wa giza ulioachiliwa kutoka kwenye miji 4 ya wakuu wa giza – yaani, Gaza, Ashdodi na Ashkeloni pamoja na Ekroni.

miungu iliweza kulifunga kabila zima. Je! Iliwezekanaje kukamata kabila lote na kulifunga? Kwa kupitia mtu mmoja (mkuu wa kabila) miungu ikalifunga kabila.

Wakuu wa giza hushughulika sana na wakuu wa makabila na Mungu nae hushughulika pia na wakuu wa kabila waliobeba kabila Fulani.Angalia vipaumbele vya kabila 12 za Israeli.

Mwanzo 49;3-4 Reubeni, u mzaliwa wangu wa kwanza, Nguvu zangu, na malimbuko ya uwezo wangu. Umewapita wengine kwa ukuu na kwa nguvu.

Umeruka mpaka kama maji, basi usiwe na ukuu, Kwa sababu ulikipanda kitanda cha baba yako, Ukakitia unajisi; alikipandia kitanda change Reuben alipozini na mke wa babaye iliharibu hatima ya kizazi chake ,nachotaka ujue Mungu huangalia waanzilishi wa kabila na si watakaofuata…mfumo wa badae wa kizazi cha Reuben uliharibika kutokana na Reuben mkuu wa kabila la Reuben.

Leo hii hayo mambo yapo hiyo ni madhabahu ya uasherati iliyowekwa na waanzilishi wa kabila lako,huenda kuna mambo ambayo hujapata ufumbuzi mpaka sasa fuatilia habari ya kabila lako na viapo vyao.Reubeni alikuwa ndiye mzaliwa wa kwanza lakini Baraka zote alipewa Yusuph nduguye,vipo viapo vingi vya kabila lako ambavyo vilikuunganisha na madhabahu ya baali na mpaka sasa inashughulika na maisha ya vizazi vyako mpka Mungu mwenyewe aingiie kati.( 1Nyakati 5:1-3. Na wana wa Reubeni, mzaliwa wa kwanza wa Israeli; (kwa maana ndiye aliyekuwa mzaliwa wa kwanza, lakini, kwa kuwa alikinajisi kitanda cha babaye, haki yake ya mzaliwa wa kwanza walipewa wana wa Yusufu, mwana wa Israeli; tena nasaba isihesabiwe kwa kuifuata hiyo haki ya mzaliwa wa kwanza.)

Kwani Yuda ndiye aliyeshinda miongoni mwa nduguze, na kwake ndiko alikotoka mtawala; bali haki

ile ya mzaliwa wa kwanza alipewa Yusufu );

(5) Jambo la tano.Kuingia katika eneo ambalo wanaabudu miungu mingine yatosha kukuunganisha na madhabahu zao

. Waamuzi 2;11-13 Wana wa Israeli walifanya yaliyokuwa ni maovu mbele za macho ya Bwana, nao wakawatumikia Mabaali.

Wakamwacha Bwana, Mungu wa

baba zao, aliyewaleta kutoka katika nchi ya Misri, wakafuata miungu mingine, baadhi ya miungu ya watu wale waliokaa karibu nao pande zote, wakajiinamisha mbele yao; wakamkasirisha Bwana, akaghadhibika.

Wakamwacha Bwana, wakamtumikia Baali na Maashtorethi. Kama umeokoka na hauna stamina ya kiimani katika Kristo ndani yako na nguvu ya Roho Mtakatifu ni rahisi sana kuruhusu madhabahu nyingine iingilie na kutawala mfumo wa maisha yako ya kiroho.Inategemea sana na nguvu ya Mungu itendayo kazi ndani yako binafsi au upako wa Mungu juu yako binafsi.

Wana wa Israel waliingia kwenye miungu ya kigeni kutokana na upako wa viongozi wao ndio maana walipoachwa walianza kuabudu miungu migeni ya madhabahu za kigeni.fuatilia tangu walipoanza safari toka Misri,kukaa kwao kiimani kulitegemea sana na imani na uimara wa kiongozi waona si wao wenyewe haijalishi waiweka maagano ya namna gani na Mungu na kwa kiwango gani.,

(6)jambo la sita.Kujiingiza kwenye agano la ndoa unaachilia mfumo mpya wa utendaji kazi ndani yako. Unapoingia kwenye suala zima la ndoa yapo mambo ya msingi sana ya rohono yakupasa ushughulikie kabla ya ndoa ili imani yako katika Kristo Yesu iwe thabiti.maana unapoingia kwenye ndoa ni agano lingine la kiamisha kwako na lina uhusiano mkubwa sana na maisha yako ya kiroho. Waamuzi 3;4-7 Naye aliwaacha ili awajaribu Israeli kwa hao, apate kujua kwamba watasikiliza amri za Bwana, alizowaamuru baba zao, kwa mkono wa Musa.

Basi wana wa Israeli wakaketi kati ya Wakanaani; hao Wahiti, na hao Waamori, na hao Waperizi, na hao Wahivi na hao Wayebusi;

wakawaoa binti zao, na binti zao wenyewe wakawaoza wana wao waume, na kuitumikia miungu yao.

Wana wa Israeli walifanya yaliyo maovu mbele za macho ya Bwana, nao wakamsahau Bwana, Mungu wao, nao wakawatumikia Mabaali na Maashtoreth .Kujiingiza kwa Waisraeli katika ndoa ilikuwa njia tosha ya kuwafunganisha na madhabahu za miungu mingine,kitendo tu cha kuoa au kuolewa yatosha kukuingiza kwenye madhabahu nyingine isipokuwa umepata ufahamu juu ya jambo hilo.

Ndoa ni eneo tosha la kubadili mfumo wako wa maisha kuwa mazuri au mabaya,Israeli waliruhusu mungu baali na maashtoreth kupitia ndoa na kila madhabahu ina Mungu wake na tabia zake.

Suleiman alipooa wanawake wa kigeni walibadili imani yake mbele ya madhabahu ya Mungu(1Wafalme 11.1-8 1 Mfalme Sulemani akawapenda wanawake wengi wageni, pamoja na binti yake Farao, wanawake wa Wamoabi, na wa Waamoni, na wa Waedomi, na wa Wasidoni, na wa Wahiti,

na wa mataifa Bwana aliyowaambia wana wa Israeli, Msiingie kwao, wala wasiingie kwenu; kwa kuwa hakika wataigeuza mioyo yenu kuifuata miungu yao. Sulemani akaambatana nao kwa kuwapenda.

Akawa na wake mia saba binti za kifalme, na masuria mia tatu; nao wakeze wakamgeuza moyo.

Maana ikawa, Sulemani alipokuwa mzee, wake zake wakamgeuza moyo wake, afuate miungu mingine, wala moyo wake haukuwa mkamilifu kwa Bwana, Mungu wake, kama moyo wa Daudi baba yake.

Kwa kuwa Sulemani akamfuata Ashtorethi, mungu mke wa Wasidoni na Milkomu, chukizo la Waamoni.

 Sulemani akafanya yaliyo mabaya machoni pa Bwana, wala hakumfuata Bwana kwa utimilifu, kama Daudi baba yake.

Sulemani akamjengea Kemoshi, chukizo la Wamoabi, mahali pa juu, katika mlima uliokabili Yerusalemu, na Moleki, chukizo la wana wa Amoni.

Na kadhalika ndivyo alivyowafanyia wake zake wa nchi za kigeni, waliofukiza uvumba, wakawatolea miungu yao dhabihu.) ”You must not intermarry with them because they will surely turn your heart after their gods..hii ni sababu tosha ya kulinda imani yako kwa Kristo ili usije ukaingia katika madhabahu za baali.na kujifunganisha kwa kutoa sadaka.

Tambua kuwa unapoanza agano la ndoa kuna kuwa na mifumo tofauti ya kiutwala katika maisha yako

Baadhi ya miungu na harakati zake juu ya makabila ya Israel 2Falme 23:13.( Nazo madhabahu zilizokuwako darini juu ya chumba cha juu cha Ahazi, wafalme wa Yuda walizozifanya, nazo madhabahu alizozifanya Manase katika behewa mbili za nyumba ya Bwana, mfalme akazivunja, akazitelemsha huko nje, na kuyatupa mavumbi yake katika kijito cha Kidroni.

Na mahali pa juu palipokuwapo mbele ya Yerusalemu, palipokuwa upande wa kuume wa mlima wa uharibifu, alipopajenga Sulemani, mfalme wa Israeli, kwa Ashtorethi, chukizo la Wasidoni, na Kemoshi, chukizo la Moabu, na Milkomu, chukizo la wana wa Amoni, mfalme akapanajisi.

kazivunja-vunja nguzo, akayakata-kata maashera, akapajaza mahali pake mifupa ya watu)

Ashtoreshi – alikuwa mungu mke wa kabila la wasidoni, kama inavyoonekana katika 1 Wafalme 11:33. Ashtoreshi ni kirefu cha “Ashera” ambaye pia aliaminiwa kuwa ni mungu anayefanikisha uzazi wa kila kitu. kwa sababu wameniacha mimi wakaabudu Ashtorethi, mungu mke wa Wasidoni, na Kemoshi, mungu wa Wamoabi, na Milkomu, mungu wa wana wa Amoni wala hawakuenda katika njia zangu, kutenda mema machoni pangu, kuzishika sheria zangu na hukumu zangu, kama Daudi baba yake.

2 Kemoshi – alikuwa mungu wa wamoabi – mungu kemoshi na baal – peori ni miungu iliyowatesa sana kabila la moabi hata kwa kuwafanya kuwa waasherati na wazinzi – Hesabu 25:1 – 3. Basi Israeli akakaa Shitimu, kisha watu wakaanza kuzini pamoja na wanawake wa Moabu;

 kwa kuwa waliwaalika hao watu waende sadakani, sadaka walizowachinjia miungu yao; watu wakala chakula, wakaisujudu hiyo miungu yao.

Ikawa Israeli kujiungamanisha na Baal-peori; hasira za Bwana zikawaka juu ya Israeli.

Kisha Bwana akamwambia Musa, Watwae wakuu wote wa hao watu, ukamtungikie Bwana watu hao mbele ya jua, ili kwamba hizo hasira kali za Bwana ziwaondokee Israeli.

 Basi Musa akawaambia waamuzi wa Israeli, Waueni kila mtu watu wake waliojiungamanisha na Baal-peori.

 Na tazama, mtu mmoja miongoni mwa wana wa Israeli akaja na kuwaletea nduguze mwanamke Mmidiani mbele ya macho ya Musa, na mbele ya macho ya mkutano wote wa wana wa Israeli, hapo walipokuwa walia mbele ya mlango wa hema ya kukutania .

3. Milkomu au moleki – alikuwa mungu wa Amoni. Moleki alilitawala na kulikandamiza kabila la waamoni. Mungu moleki ndiye aliyelifanya kabila la waamoni kuamini kwamba, wakitoa sadaka ya kafara ya watoto watafanikiwa na kuwa karibu na mungu – Lawi 20:1 – 5( Kisha Bwana akanena na Musa, na kumwambia,

Tena uwaambie wana wa Israeli, Mtu awaye yote miongoni mwa wana wa Israeli, au miongoni mwa wageni waketio katika Israeli, atakayetoa katika kizazi chake na kumpa Moleki, sharti atauawa; wenyeji wa nchi watampiga kwa mawe.

 Mimi nami nitamkazia uso wangu mtu huyo, nami nitamkatilia mbali na watu wake; kwa kuwa ametoa katika kizazi chake na kumpa Moleki, ili kupatia unajisi patakatifu pangu, na kulinajisi jina langu takatifu.

Tena kama wenyeji wa nchi wakimfumbia macho mtu huyo kwa njia yo yote, hapo atoapo katika kizazi chake na kumpa Moleki, wasimwue;

dipo mimi nitamkazia uso wangu mtu huyo, na jamaa zake, nami nitamkatilia mbali, na hao wote wamwandamao katika uzinifu, ili kufanya uzinifu pamoja na Moleki, watengwe mbali na watu wao)

2Falme 17:17 ndiye anayeongoza ibada za sadaka za watoto mpaka leo, na sadaka za mimba changa. Sulemani alipomuoa mke wa Amoni bila kujua miungu ya chimbuko lake, ghafla nafsi yake ilinaswa katika ulimwengu wa giza na akaanza kujenga madhabahu kwa ajili ya mungu Moleki. Na kuanzia hapo miungu 4 ilianza kummiliki – 1Falme 11:5 -7.

Unaposoma 1Falme 11:3-8” Akawa na wake mia saba binti za kifalme, na masuria mia tatu; nao wakeze wakamgeuza moyo.

Maana ikawa, Sulemani alipokuwa mzee, wake zake wakamgeuza moyo wake, afuate miungu mingine, wala moyo wake haukuwa mkamilifu kwa Bwana, Mungu wake, kama moyo wa Daudi baba yake.

Kwa kuwa Sulemani akamfuata Ashtorethi, mungu mke wa Wasidoni na Milkomu, chukizo la Waamoni.

 Sulemani akafanya yaliyo mabaya machoni pa Bwana, wala hakumfuata Bwana kwa utimilifu, kama Daudi baba yake.

Sulemani akamjengea Kemoshi, chukizo la Wamoabi, mahali pa juu, katika mlima uliokabili Yerusalemu, na Moleki, chukizo la wana wa Amoni.

a kadhalika ndivyo alivyowafanyia wake zake wa nchi za kigeni, waliofukiza uvumba, wakawatolea miungu yao dhabihu. ”

Unagundua kuwa, nafsi ya Mfalme Sulemani ilifungwa pingu na miungu 4.

Ashtoreshi – mungu mke wa wasidoni

Milkomu au moleki – mungu wa Waamoni

Kemoshi – mungu wa Wamoabu

Baal – miungu ya Wafilisti ambayo aliitolea sadaka.

)Jambo la saba.Maagano ya kinadhiri yaliyoweka wakati ukiwa tumboni mwa mama yako au kabla hata ya wewe katika ulimwengu huu wa mwili. Hili ni jambo linine ambalo linatosha kabisa kukufunganisha kabisa na madhabahu Fulani.Wapo wazazi kabla ya wewe kuzaliwa wa huenda wanaipitia eneo gumu la kukupata wewe,wanafikia sehemu ili uzaliwe wanaweka agano la kinadhiri kwa miungu Baali au Mungu aliyehai hivyo kiroho kwa namna moja au nyingine unakuwa umeunganishwa na madhabahu husika kabla yaw ewe kuzaliwa.Nimeona watu wanapata matatizo ambayo yanatokana na madhara ya wao kuunganishwa kwenye madhabahu za miungu baali na maisha yao yanakosa muelekeo kwa sababu uhai wa maisha yao ya badae umefungwa katika madbahahu ya miungu baali.Kadhalika kwa Mungu pia ni hivyo hivyo,Tazama habari za Hana kabla ya Samweli kuzaliwa alikwisha muunganisha na madhabahu ya Mungu(1Samweli 1:11 Then she made a vow and said,O Lord of hosts if you will indeed look on tha afflication of your maidservant and remember me and not forget your maidservant,but will give your maid servant a MALE CHILD then I will give him to the Lord all days of his life and no razor shall come upon his head”)hiyo lilikuwa agano la kinadhiri ambalo ilimsababisha Mungu kumjibu Hana na kuzaliwa kwa mtoto mume Samweli na badae anampeleka madhabahuni kwa kuhani Eli angalia na jina alilompa mwanae,lilikuwa na muunganiko kiroho na agano ambalo aliweka kwenye madhabahu ya Mungu na Mungu anapata nafasi ya kupitisha nguvu zake hapo kwa ajili ya taifa la Israeli(1samweli 1:22) kwa hiyo ni vema sana ukajua namna ya mfumo mzima wa wewe kuzaliwa na kaa na wazazi wako uwaulize habar zako kabla yaw ewe kuzaliwa,wapo wanaotaka wazaliwa wao wa kwanza wamtumikie Mungu na ndio maana unajikuta upo nyumbani mwa Mungu na vita vyake vya rohoni si vya kawaida.

NAMNA GANI UTAJINASUA NA MIUNGU BAALI?

Mruhusu Mungu Akupe maeneo ya kushughulikia kimaombi maana usiende kwa namna unavyofikiri kushulika na madhabahu nyingine maana inahitaji sana nguvu za MUNGU

Hili jambo si la kawaida na si krahisi kwa sababu ya vitu vilivyowekwa na kukuunganisha na madhabahu za miungu baali.Tazama nami Waamuzi 6;25 Maelekezo anayoyapokea Gideon juu ya kuvunja madhabahu za baali amtwae ng’ombe maana yake kuwa sadaka ya Damu kwa agano la kale lakini sasa ipo Damu ya Yesu pekee ya kukutoa katika maagano hayo ya miungu baali yanayoshikilia mfumo mzima wa maisha yako’sasa kila madhabahu inatabia na mifumo yao na Mungu pekee ndie atakayetoa ufahamu na maarifa ya kutoka huko kwenye madhabahu za baali.

Madhabahu zinaweza wakilishwa na vitu mbalimbali mfano miti mikubwa(mwanzo 21;33),kwenye milima(kutoka 3:12 Yohana 4:20)ndio maana yakupasa uombe muongoze kwa Mungu mwenyewe namna ya kutoka huko.

Upo uhusiano mkubwa sana kati ya maisha yako binafsi na madhabahu husika na kila moja inafumo wake. Angalia madhabahu aliyoibeba Yesu kipindi anazaliwa Je ulishawai kujiuliza kwa nini Herode aliagiza watoto wa miaka miwili tena wakiume wauawe?Ukienda pasipo utaratibu wa Mungu juu ya madhabahu ulioko,kujinasua italetashida isipokuwa kwa njia y Yesu tu

Ndani ya Yesu kulikuwa na mfumo wa kitwala kifalme rohoni na ulimwengu wa nyama

Mifumo miwili ya kiutawala yenye kutofautiana kiitifaki haiwezi kukaa pamoja hata siku moja.

MUNGU AKUBARIKI SANA NA AKUPE UFAHAMU NA UELEWA ZAIDI JUU YA MASUALA MAZIMA YA MADHABAHU# By prophet of God