MAMBO YAKUUNGANISHAYO NA MADHABAHU HUSIKA .
(1)Jambo la kwanza;SADAKA.
Sadaka ni njia mojawapo ya kuunganisha maisha yako mwenyewe na wewe mwenyewe na vizazi vyako katika madhabahu husika ndio maana Yesu alifanyika sadaka ili tuwe na mamlaka na ukuhani katika Ufalme wa Mungu Ebrania :28” na kadhalika Kristo naye, akiisha kutolewa sadaka mara moja azichukue dhambi za watu wengi; atatokea mara ya pili, pasipo dhambi, kwa hao wamtazamiao kwa wokovu”
Chunguza katiaka ukoo wako kabila ni muda gani wanatoa sadaka na kwa sababu gani?Uthamani wa sadaka ndio nguvu ya miungu ya madhabahu husika.Waamuzi 6:25-32 Gideoni alitoa sadaka ili kuwatoa wana wa Israeli katika miungu Baali na kuwaunganisha na madhabahu ya MUNGU pasipo wao kujua ndio maana inaleta shida mara baada ya kugundua mungu wa baali hayupo.Na kila sadaka inautaratibu wake kulingana na nini na kitu gani kinakusudiwa kitokee ndio maana ukienda kwa waganga wa uchawi wana aina tofauti tofauti ya sadaka kutokana na matokeo unayoyahitaji,kadhalika kila madhabahu ina mungu wake na mfumo wake.
Ukisoma Waamuzi 6:29-30
Wakaambiana, Ni nani aliyetenda jambo hili? Hata walipotafuta habari na kuuliza, wakasema, Gideoni, mwana wa Yoashi, ndiye aliyetenda jambo hili.Ndipo watu wa mji wakamwambia Yoashi Mlete mwanao, afe; kwa sababu ameibomoa madhabahu ya Baali na kwa sababu ameikata ile Ashera iliyokuwa karibu nayo Angalia kuitoa madhabahu ya baali ilisababisha ugomvi juu yao kwa sababu “ameikata”maana yake amewatenga na miungu baali ya kwao na kuwaunganisha na MUNGU aliye hai.Mifumo ya kiutawala ya kwao ilitawaliwa na Miungu migeni ndio maana kila mtawala wa wakati ule Israeli alijiunganisha na miungu baali.
Maisha yako namna yalivyo inawezekana kabisa ulifungwa kwenye sadaka na kutolewa kwenye madhabahu Fulani,we chunguza habari ya maisha mlionayo.Unaweza ukaingizwa kwenye mungu wa madhabahu fualani pasipo wewe kujua badala yake utaona mabadiliko katika mfumo wa maisha yako.”Kuondolewa kwa madhabahu ya baali iliinua vita vingine si kwa sababu madhabahu iliondolewa la hasha,bali mfumo wa maisha ya kiutawala juu ya Israeli umebadilishwa Ezra 3:3 Hata ulipowadia mwezi wa saba, na wana wa Israeli walipokuwa katika miji yao, watu wakakusanyika pamoja huko Yerusalemu kama mtu mmoja.
Ndipo akasimama Yoshua, mwana wa Yosadaki, na ndugu zake makuhani, na Zerubabeli, mwana wa Shealtieli, na ndugu zake, nao wakaijenga madhabahu ya Mungu wa Israeli, ili kutoa sadaka za kuteketezwa juu yake, kama ilivyoandikwa katika torati ya Musa, mtu wa Mungu.
Wakaiweka madhabahu juu ya msingi wake; maana hofu imewashika kwa sababu ya watu wa nchi; wakamtolea Bwana sadaka za kuteketezwa juu yake, sadaka za kuteketezwa za asubuhi na jioni. Mfumo wa maisha ya Israeli ilisababisha watoe sadaka itakayowaunganisha na Mungu aliye hai ndio maana wakakusanyika pamoja Je upo kwenye madhabahu gani inayoamua maisha yako?
(2) Jambo la pili:Majina uliyopewa yanaweza kabisa kukuunganisha na miungu wa madhabahu Fulani.wengi wana majina lakini hawajui asili ya majina yao.
Palipo na jina hapo ndipo kuna utambulisho wa mtu katika vision yake na mfumo mzima wa maisha yako.Adamu alipewa mamlaka ya kuwapa majina viumbe walioumbwa na Mungu kwa nini,sababu moja wapo utambulisho wao katoka ulimwengu war oho upo kwenye majina.kadhaliaka future yako inauhusiano mkubwa sana na jina ulilonanlo sasa.Jamii nyingi hapa wanatabia ya kurithishana majina wakiamini mhisika bado yupo na hapo ndipo unapounganishwa na miungu ya kikabila na kiukoo na mfumo wako wa maisha utakuwa chini ya madhabahu hizo za kiukoo,na maono yako yamefichwa huko hata kama umeokoka (mwenye maarifa na afahamu)Mwanzo 2:19-20 . Bwana Mungu akafanyiza kutoka katika ardhi kila mnyama wa msituni, na kila ndege wa angani, akamletea Adamu ili aone atawaitaje; kila kiumbe hai, jina alilokiita Adamu likawa ndilo jina lake.
Adamu akawapa majina yao kila
mnyama wa kufugwa, na ndege wa angani, na kila mnyama wa mwituni; lakini hakuonekana wa kumsaidia Adamu aliyefanana naye.
Yakobo nae alibadilishwa utambulisho wake na kuitwa Israeli maana yake mbarikiwa na Ibrahimu pia kwa nini? Future ya mtu ina uhusiano mkubwa na jina la mtu,kadhalika na madhabahu zinahusika kabisa na mfumo wote wa maisha ya mtu hivyo jina ulilonalo yatosha kabisa kuunganishwa na miungu wa madhabahu husika.Angalia baada ya Abraham kuitwa Ibrahimu Mungu anamwambia maana ya jina lake,,yaani limebeba nini hapo badae,Mwanzo 17:6-8
Hivyo madhabahu Fulani inatambua vision yako hapo baadae na kwa kuwa ni chanzo au eneo ambalo linatawala mfumo mzima wa maisha yako hapo badae basi jina lako linaweza likaunganishwa na madhabahu fualani.Ndio maana kila jina lina maana si kawaida ila ni utambulisho wa roho iliyoko kwenye majina Jina lako au maana ya uhai wako upo kwenye nafsi na nafsi imebeba uhai wako(Roho Mtakatifu akufunulie hili jambo)nafsi ikifa uhai wako haupo,kadhalika miungu ya giza hushughulika sana na nafsi ya mtu kama ndivyo utambulisho wako upo ndani ya nafsi na nafsi imeficha jina lako hapo,Basi jina lako ni njia mojawapo ya kuunganishwa na madhabahu husika.
(3) jambo la tatu.Maagano yaliyowekwa mwanzoni yatosha kukuunganisha na madhabahu za giza Je kuna maagano mangapi nay a aina gani ambayo wazazi wako waliweka wakati unazaliwa aidha kupitia kitovu au damu yako au nywele zako,zilifungwa kwenye miungu gani?si suala la kujiuliza mpendwa. Yapo maagano ya aina nyingi,lakini agano la damu ni agano lenye nguvu kwa sababu damu ina sauti,uhai,na damu inatoa laana,Ebra,12:24,Lawi 17;10-12.Kumbuka yapo maagano ya Damu yaambatanayo na sadaka kwa ajili ya ibada za miungu migeni.
Hivyo damu pia inahusika kabisa katika kuamua maisha yako ya badae kulingana na maagano yaliyoko katika damu na wewe.Ndio maana wachawi nao hupenda sana kutumia damu kwa ajili ya kukamata mfumo wa maisha ya mtu ,nafsi katika madhabahu zao.
Madhabahu nyingi zinakuwa na Nguvu kutokana na maagano ya damu.Angalia nabii Eliya alivyounganisha kabila 12 za majina katika Israeli na damu pia.hivyo damu inatosha kabisa kukuunganisha na madhabahu Fulani. (1Wafamle 18:32-35 Naye akaijenga madhabahu kwa mawe hayo katika jina la Bwana; akafanya mfereji, kama wa vipimo viwili vya mbegu, ukiizunguka madhabahu.
Kisha akazipanga zile kuni, akamkata yule ng'ombe vipande vipande, akaviweka juu ya kuni. Akasema, Jazeni mapipa manne maji, mkayamwage juu ya sadaka ya kuteketezwa, na juu ya kuni.
Akasema, Fanyeni mara ya pili. Wakafanya mara ya pili. Akasema, Fanyeni mara ya tatu. Wakafanya mara ya tatu.
Yale maji yakaizunguka madhabahu; akaujaza mfereji maji.) Eliya alifanya hivyo kulingana na uhusika wa madhabahu,na majina Damu na sadaka Mapipa manne,pande nne za Israeli,wakajaza maji na kumwaga juu ya juu ya sadaka ya kuteketezwa,mara tatu hesabu yake ni 12 saw na akbila 12 za Israeli kutoka pande nne za dunia,kiroho maji damu zinashuhudia hapa duniani
(1Yoh 5:9) na ndani ya sadaka kuna damu na maji na majina ya isreali KIKABILA juu ya madhabahu,kwa mantiki hiyo Majina ya Israeli yalifungwa kwenye madhabahu na sadaka zake na katika sadaka kuna Damu iliyomwagia katika hiyo madhabahu ya MUNGU.
Watu wengi mfumo wao wa kimaisha unayumba kutokana na maagano ya damu yaliyowekwa kwenye madhabahu husika ambayo yamefunga maisha yao katika madhabahu za miungu yao.Wengi huenda hawajua yakupasa ujue utaratibu wa ukoo wenu na historia ya ukoo wako ili ujue namna ya kutoka huko.Binafsi ilinigharimu miaka miwili ya maombi kuombea maagano na familia yangu kiujumla kwa uwezo wa Roho
Mtakatifu.
Tazama name kipindi cha Nuhu,mara baada ya gharika jambo la kwanza Nuhu kufanya ni kumjengea Mungu madhabahu ili mfumo mpya wa kizazi kilichobakia uwe ndani ya madhabahu ya Mungu(Mwanzo 8:20-22. Nuhu akamjengea Bwana madhabahu; akatwaa katika kila mnyama aliye safi, na katika kila ndege aliye safi, akavitoa sadaka za kuteketezwa juu ya madhabahu.
Bwana akasikia harufu ya kumridhisha; Bwana akasema moyoni, Sitailaani nchi tena baada ya hayo kwa sababu ya wanadamu, maana mawazo ya moyo wa mwanadamu ni mabaya tangu ujana wake; wala sitapiga tena baada ya hayo kila kilicho hai kama nilivyofanya.
Muda nchi idumupo, majira ya kupanda, na mavuno, wakati wa baridi na wakati wa hari, wakati wa kaskazi na wakati wa kusi, mchana na usiku, havitakoma. Mungu atasema Baraka juu ya maisha yao na majira na nyakati katika mfumo mpya wa maisha,yote hayo ni baada ya kutoa sadaka ya damu juu ya madhabahu ya Mungu(akatwaa katika kila mnyama aliye safi, na katika kila ndege aliye safi, akavitoa sadaka za kuteketezwa juu ya madhabahu.) Mungu anasema “ Sitailaani nchi tena baada ya hayo kwa sababu ya wanadamu, maana mawazo ya moyo wa mwanadamu ni mabaya tangu ujana wake; wala sitapiga tena baada ya hayo kila kilicho hai kama nilivyofanya.”maana yake anaachilia Baraka katika mfumo mpya wa maisha yao.
- Madhabahu zimekamata mfumo mzima wa utawala wa maisha ya mt