NAMNA MADHABAHU ZINAVYOWEZA KUSHIKILIA MFUMO WAKO WA MAISHA

NENO :Waamuzi 6:24

“Ndipo Gideoni akamjengea Bwana madhabahu hapo, akaiita jina lake, Yehova-Shalomu; hata hivi leo iko huko katika Ofra ya Waabiezeri.”

Madhabahu ni eneo ambalo linaweza kutumia na Mungu au shetani ili lijengwe kwa kupitisha nguvu ,mamlaka na utawala wake na kila madhabahu ina tabia zake.

Madhabahu ni eneo ambalo linakuwa daraja kutoka ulimwengu war oho kupitisha kilichokusudiwa hadi ulimwengu wa mwili au nyama.NAmadhabahu

zinatenda kazi kulingana na utawala na mfumo wa mmiliki wao.au kwa lugha nyingine madhabahu ni eneo litumiwalo na watu watu Fulani kwa ajili ya kufanya ibada zao wakiwa na imani ya nguvu ya pale,mungu wa eneo lile kulingana na utaratibu wa lile eneo na kila madhabahu zinategemea na utendaji wa roho wa eneo lile au miungu wa madhabahu husika.Zipo madhabahu za aina mbili au zenye utawala wa namna mbili,

A)Madhabahu ya MUNGU.

B)Madhabahu ya shetani.

Ili hizi madhabahu zifanye kazi zinategemea sana

Mungu wa madhabahu

Nguvu ya madhabahu

Sadaka zitolewazo madahahu husika

Nguvu ya kuhani husika

Sadaka zitolewazo katika madhabahu husika

zinauhusianao mkubwa sana na nguvu itokayo katika madhabau husika juu ya mfumo husika wa maisha yako na maono uliyobeba juu ya maisha yako ya badae.Na madhabahu ya MUNGU au ya shetani zote zinafanya kazi kulingana na ene lililopo katika ulimwengu wa roho yani kulingana na itifaki ya kiutawala juu ya madhabafu husika au mahali pa juu husika katika ulimwengu war oho.(Yeremia 32.35 “Tena walijenga mahali palipoinuka kwa Baali, palipo katika bonde la mwana wa Hinomu, ili kuwapitisha wana wao na binti zao katika moto kwa ajili ya Moleki, jambo nisilowaagiza; wala halikuingia moyoni mwangu kwamba walitende chukizo hilo; wapate kumkosesha Yuda ”)

(Waamuzi 6;26 “ukamjengee Bwana, Mungu wako, madhabahu juu ya ngome hii, kwa taratibu zake; ukamtwae yule ng'ombe wa pili na kumtoa awe sadaka ya kuteketezwa, kwa kuni za ile Ashera uliyoikata ”

Kwa hiyo kila mabdhabahu inataratibu zake na sadaka zake na ina toa matokeo kulingana na sadaka zitolewazo katika madhabahu husika. ANGALIZO . “NGUVU YA MADHABAHU HUTEGEMEA SANA KIWANGO CHA SADAKA ITOLEWAYO KATIKA MADHABAHU HIYO.” Matendo:10;2-4 Kornelio alikuwa amebeba madhabahu ya Mungu na sadaka zake zilisababisha nguvu za Mungu katika madhabahu ya Munguiliyokuwa ndani yake zitoe majibu ya maombi yake ya Muda mrefu mbele za Mungu,,ulishawahi kujiuliza kama angekata tamaa kutoa sadaka nyingi ingekuwaje?

“Akamtazama sana, akaogopa akasema, Kuna nini, Bwana? Akamwambia, Sala zako na sadaka zako zimefika juu na kuwa ukumbusho mbele za Mungu.

Sasa basi, peleka watu Yafa, ukamwite Simoni, aitwaye Petro .”hii ina maana kuwa sala zako ziambatanazo na sadaka katika madhabahu yangu zimefika kikamilifu na sasa majibu ya maombi yako yanatoaka mahali pangu pa juu..(madhabahu ya Mungu)

Hivyo basi nguvu ya madhabahu kukupa majawabu ya maombi yako inategemeana sana na sadaka unazotoa katika madhabahu.Madhabahu ni daraja kati yako inayopitisha vitu kati yako na Mungu unayemtumkia.Swali la kujiuliza jee unajua upo katika madhabahu gani hata kama umeokoka? yawezekana hata kama umeokoka bado umevaa Sanda (nguvu ya madhabahu Fulani)Maana haikutosha tu kufufuliwa kwa Lazaro na Yesu mpaka ilipotolewa amri ya kumvua sanda..haitoshi ya kuwa wewe tayari unatiketi ya kwenda mbinguni,,,Je mfumo wa maono uliyobeba yanakwendaje..vipi elimu ipo sawa sawa..maendeleo yako ya kiuchumi yapo sawasawa..suala la ndoa jee limekaa sawasawa?(Yohana 11.43-44)

Ngoja kushirikishe hili, SADAKA YA MADHABAHU

Kiitifaki sadaka zitolewazo madhabahu Fulani huwa zinahuisha na kutiisha nguvu ya madhabahu hiyo.Kama upo katika madhabahu ya Mungu aliye hai unaambatanishwa na vitu vitano ambavyo ndani yake kuna mfumo mzima wa kiiutawala juu ya maisha yako na maono uliyonayo.Unaambatanishwa na,

Mungu wa madhabahu

Nguvu ya madhabahu

Sadaka za madhabahu

Ibada za eneo hilo

Na kuhani wa madhabahu hiyo.

Ukisoma mwanzo 8;,20-22.”

Nuhu akamjengea Bwana madhabahu; akatwaa katika kila mnyama aliye safi, na katika kila ndege aliye safi, akavitoa sadaka za kuteketezwa juu ya madhabahu.

Bwana akasikia harufu ya kumridhisha; Bwana akasema moyoni, Sitailaani nchi tena baada ya hayo kwa sababu ya wanadamu, maana mawazo ya moyo wa mwanadamu ni mabaya tangu ujana wake; wala sitapiga tena baada ya hayo kila kilicho hai kama nilivyofanya.

Muda nchi idumupo, majira ya kupanda, na mavuno, wakati wa baridi na wakati wa hari, wakati wa kaskazi na wakati wa kusi, mchana na usiku, havitakoma .”utaona kabisa Sadaka aliyoagizwa Nuhu atoe zinaachilia mfumo mpya wa maisha yao na ndani yake kuna ibada,sadaka,nguvu ya madhabahu,kuhani na Mungu mwenyewe.

Madhabahu zote huanzishwa katika ulimwengu war oho na utendaji wake kuwepo katika ulimwengu wa kawaida au wa nyama.

Madhabahu zinatoa maelekezo ya mfumo wa maisha yako kwa kujua au kutokujua ndio maana yapo makabila mengi hapa Tanzania ambayo yana muda maalumu wa kutoa sadaka ila mambo yao yaendea sawia,we unafikiri ni hali ya kawaida la hasha! Mfumo wako wa maisha umefungwa kwenye madhabahu .

Madhabahu ya ulimwengu war oho huunganishwa na madhabahu za ulimwengu wa nyama kupitia

Sadaka

Makuhani

Ibada zifanyikavyo kwa wakati.

MAMBO YAKUUNGANISHAYO