Mwanzo 8:15-22 “Mungu akamwambia Nuhu, akisema,Toka katika safina, wewe, na mkeo, na wanao, na wake za wanao pamoja nawe.Utoe pamoja nawe kila kilicho hai kilichomo pamoja nawe, chenye mwili, ndege, na mnyama, na kila kitambaacho, chenye kutambaa juu ya nchi; wajae katika nchi, wawe na uzazi, wakaongezeke katika nchi.Basi Nuhu akatoka, yeye, na wanawe, na mkewe, na wake za wanawe pamoja naye;kila mnyama, na kila kitambaacho, na kila ndege, kila kinachokwenda juu ya nchi kwa kabila zao, wakatoka katika safina. Nuhu akamjengea Bwana madhabahu; akatwaa katika kila mnyama aliye safi, na katika kila ndege aliye safi, akavitoa sadaka za kuteketezwa juu ya madhabahu. Bwana akasikia harufu ya kumridhisha; Bwana akasema moyoni, Sitailaani nchi tena baada ya hayo kwa sababu ya wanadamu, maana mawazo ya moyo wa mwanadamu ni mabaya tangu ujana wake; wala sitapiga tena baada ya hayo kila kilicho hai kama nilivyofanya.”

Hii ni madhabahu ya familia ya Nuhu, wakati wa kizazi cha Nuhu watu walikua wamebadilika kwa kutenda maovu Mungu akaamua kuondoa uharibifu huo kwa kupitia Nuhu, Mungu hawezi kutenda jambo bila kuwajulisha watu wake, Mungu alimwambia Nuhu awaambie watu wabadilike lakini watu hawakumsikililiza ndipo akamwambia ajenge safina na kuwaingiza viumbe wote wawili wawili ndani yake pamoja na familia ya Nuhu, na wanawe, Mungu akaiangamiza dunia na wakabaki watu nane ambao baada ya kubaki Nuhu akaamua kujenga madhabahu ikasimama kwenye familia yake.

Madhabahu nyingine ni madhabahu ya Abrahamu, Biblia inasema Ibrahimu alipokwenda wakaldayo Mungu akamtokea njiani ndipo Ibrahimu akajenga madhabahu kwaajili ya Bwana, maana yake kuna uhusihano kati ya Ibrahimu na uzao wake kwa Mungu. Ibrahimu akaweka madhabahu kati ya Mungu na familia yake.

Mwanzo 12:7 Bwana akamtokea Abramu, akasema, Uzao wako nitawapa nchi hii. Naye huko akamjengea madhabahu Bwana aliyemtokea.”

Madhabahu nyingine ni madhabahu ya Yoashi. Yoashi alikua kuhani wa Mungu lakini baadaye aliasi akaingia kwenye mambo mengine ambayo sio sawa, Biblia inasema Yoashi akajenga madhabahu ya baali ambayo yeye alikua kuhani wa madhabahu ile maana yake yeye pamoja na familia yake walikua sehemu ya madhabahu hiyo.

Waamuzi 6:25-26 “Ikawa usiku uo huo Bwana akamwambia, Mtwae ng'ombe wa baba yako, yaani ng'ombe wa pili, wa miaka saba, ukaiangushe madhabahu ya Baali, aliyo nayo baba yako, ukaikate Ashera ile iliyo karibu nayo; ukamjengee Bwana, Mungu wako, madhabahu juu ya ngome hii, kwa taratibu zake; ukamtwae yule ng'ombe wa pili na kumtoa awe sadaka ya kuteketezwa, kwa kuni za ile Ashera uliyoikata.”

Gideoni alikuwa sehemu ya madhabahu ya baba yake (ya kichawi) akawa ananyonywa nguvu, akawa hana uwezo wa kufanya jambo lolote kwasababu ya madhabahu ya baba yake lakini Mungu akaamua kuingilia kati kwasababu alikua anampango na Gideoni. Mungu huingilia kati kwenye taabu yako anapokua na mpango na wewe, Mungu aingilie kati kwenye tatizo lako kwa jina la Yesu.

Ukoo huwa unaanza na familia, familia ni kati ya Baba na mama na watoto, familia nyingi huwa sehemu ya kitu kimoja kutengeneza ukoo, watu wa kale walikua hawawezi kwenda mbele mpaka wamejenga madhabahu. Ndivyo ilivyo kanuni ya kufanikiwa huwezi kufanikiwa bila kuwa na madhabahu inayokuongoza rohoni.

Familia nazo zipo vilevile haziwezi kwenda mahala popote kama mfumo wao wa maisha umeshikiliwa kwenye madhabahu za kichawi, inawezekana familia au ukoo umeshikiliwa na mfumo wa madhabahu, ndiomaana matatizo ya ukoo wako yanafanana, kusoma kunafanana, kwenye ndoa kunafanana, kuugua kunafanana, kufanikiwa kunafanana kwasababu ya madhabahu.

Waamuzi 6:24 “Ndipo Gideoni akamjengea Bwana madhabahu hapo, akaiita jina lake, Yehova-Shalomu; hata hivi leo iko huko katika Ofra ya Waabiezeri.”

Gideoni kabla hajaenda kuibomoa madhabahu ya baba yake alijenga madhabahu akaiita jina la Jehova shalom (maana yake Mungu wa amani) familia yake imetapakaa amani. Ni vizuri kujua kwamba je madhabahu unayokwenda kuabudu unamjua anayeabudiwa hapo? ni vizuri ujue kwamba madhabahu yoyote yupo mungu anayeabudiwa hapo, huwezi kuzifahamu kwa rangi lakini unatakiwa ujue zipo madhabahu za Mungu Yehova na za shetani.

Madhabahu ni eneo ambao linaweza kutumiwa na Mungu Yehova au shetani(miungu) ili kupitisha nguvu, utawala na mamlaka kwa watu wanaokusanyika mbele yake. Madhabahu inaweza kuwa ndani ya mtu kwenye familia, unakuta Mtu kwenye familia haguswi yupo anaishi kivyake haeleweki kumbe ni madhabahu ya familia au eneo Fulani.

Matendo ya Mitume 16:17-24 “Akamfuata Paulo na sisi akipiga kelele, akisema, Watu hawa ni watumishi wa Mungu aliye juu, wenye kuwahubiria njia ya wokovu. Akafanya hayo siku nyingi. Lakini Paulo akasikitika, akageuka akamwambia yule pepo Nakuamuru kwa jina la Yesu Kristo, mtoke huyu. Akamtoka saa ile ile. Basi bwana zake walipoona ya kuwa tumaini la faida yao limewapotea, wakawakamata Paulo na Sila, wakawakokota mpaka sokoni mbele ya wakuu wa mji; wakawachukua kwa makadhi, wakasema, Watu hawa wanachafua sana mji wetu, nao ni Wayahudi; tena wanatangaza habari ya desturi zisizokuwa halali kwetu kuzipokea wala kuzifuata, kwa kuwa sisi tu Warumi. Makutano wote wakaondoka wakawaendea, makadhi wakawavua nguo zao kwa nguvu, wakatoa amri wapigwe kwa bakora. Na walipokwisha kuwapiga mapigo mengi, wakawatupa gerezani, wakamwamuru mlinzi wa gereza awalinde sana. Naye akiisha kupata amri hii akawatupa katika chumba cha ndani, akawafunga miguu kwa mkatale.”

Tunaona mtu huyu alipotolewa mapepo mji mzima ulitaharuki kwasababu msichana Yule alikua ni madhabahu ya mji mzima ambao alikua anawapa utajiri wafanya biashara. Tunaona kumbe mtu anaweza akawa ni madhabahu ya mji mzima anaunufaisha mji anaungamanika na watu wa ngazi ya juu mpaka chini.

Wapo watu ambao wakitaka kufanya jambo hawawezi kufanya hivihivi kabla hawajamuuliza mtu ambaye ni madhabahu ya eneo Fulani, mfano mtu akitaka kugombea ubunge, udiwani, utawala hawezi kufanya kabla hajamuuliza mtu huyo, Mfalme Daudi alikua akitaka kwenda vitani anamuuliza Mungu aende au asiende na akienda atawapata/shinda na Mungu alikua akimwambia nenda utashinda.

Wachawi wanajeuri sio kwasababu wamekula chakula na kushiba hapana, ni kwasababu wanaijua kesho yao kichawi ndiomaana unakuta mtu anakuambia wewe utamfanya nini? huwezi kumbabaisha kwasababu amekuchungulia rohoni na kuona hauna madhara yeyote juu yake, ni kwasababu ya madhabahu anayoitegemea uimempa taarifa za kesho yake.

Kazi ya Madhabahu ni kujibu malalamiko ya watu na kutoa ufumbuzi. Kuna madhabahu za kutatua matatizo ya watu na kila madhabahu ina eneo lake.

2 Mambo ya Nyakati 6:1-42

Madhabahu hii aliyoijenga Mfalme Suleiman tunaona ni mahala ambapo Mungu ameliweka jina lake na macho yake na masikio yake ili asikilize malalamiko ya watu wanaoyapeleka kwenye madhabahu na kutatua matataizo yao. Madhabahu za Mungu zipo kwaajili ya kuwasaidia watu, Mungu amewafundisha watu namna ya kumwendea yeye.

Ili madhabahu hizi zitende kazi zinategemeana na:-

1. Mungu wa madhabahu.

2. Nguvu ya madhabahu.

3. Kafara ya madhahu. Kafara inayotolewa ndio nguvu ya madhabahu

4. Kuhani wa madhabahu.

Madhabahu huwa haitoi matokeo kama hakuna Mungu wa madhabahu, nguvu ya madhabahu, kafara ya madhabahu, na kuhani wa madhabahu. Mfumo husika wa maisha yako au maono yako unategemeana na mahali uliposhikwa na madhabahu hiyo.

Ndiomaana kuna madhabahu inafanya kazi juu ya mtu ili aonekane wa aina Fulani. Unaweza kumkuta mtu amevaa nguo zimechanikachanika lakini ndiye anaonekana anang’aa lakini wewe umekaa unavaa vizuri ila hakuna mtu anayekuona umeng’aa ni kwasababu ya madhabahu ya mtu huyo imemfanya aonekane amependeza mbele za watu, ukiona mtu anaenda mbele au anarudi nyuma maana yake kuna madhabahu iliyomfanya arudi nyuma.

Wewe ni shujaa shida na matatizo yaliyokukamata ni kutokana na madhabahu iliyokushikilia, kuna ripoti umepewa nyingi kutoka kwa watawala, kutoka kwa wachumi, kutoka kwa wafanya biashara, kutoka kwa madaktari, kutoka kwa watu mbalimbali zile ripoti achana nazo sababu ipo madhabahu ya Mungu imesimama inataarifa ya Bwana juu ya maisha yako wewe, ripoti hii imekuja kugeuza maisha yako imekuja ili uwe shujaa juu ya maisha yako kwa jina la Yesu.

“kwa jina la Yesu leo ninavunja kila madhahu, illiyoshikilia maisha yangu kwa damu ya Yesu” Amen

Yeremia 22:9-11 “Ndipo watakapojibu, Ni kwa sababu waliliacha agano la Bwana, Mungu wao, wakaabudu miungu mingine, na kuitumikia.Msimlilie aliyekufa, wala msimwombolezee, Bali mlilieni huyo aendaye zake mbali; Kwa maana yeye hatarudi tena, Wala hataiona nchi aliyozaliwa.”

Waamuzi 6:6 “Israeli walitwezwa sana kwa sababu ya Wamidiani; nao wana wa Israeli wakamlilia Bwana.”

Madhabahu inapata nguvu kutokana na kafara ya madhabahu iliyotolewa. Umeona madhabahu ya amaleki ilikua inapitisha amaleki, nguvu ya madhabahu husika inategemea karafa iliyolewa kwenye hiyo madhabahu. Sadaka kwenye madhabahu inanguvu sana na mafanikio ya mtu, “ukitoa sadaka ya ulegevu utapokea majibu ya ulegevu”. Eliya hakutolewa kwa sadaka lakini ndege alitoka mbinguni akampa mkate na gudulia la maji akaishi. Usitende kama wanavyotenda watu wa dunia hii na wala usifikiri kama wanavyofikiri watu wa dunia hii.

Kwenye Biblia Kuna mtu na mkewe walijadiliana watoe sadaka pungufu Mungu akawatoa uhai wao ili tujifunze nguvu ya sadaka ilivyo, sadaka ina nguvu na inapotolewa haiendi kwenye mikono ya watu bali inakwenda kwa Mungu.

Matendo ya Mitume 10:1-6 “Palikuwa na mtu Kaisaria, jina lake Kornelio, akida wa kikosi kilichoitwa Kiitalia, mtu mtauwa, mchaji wa Mungu, yeye na nyumba yake yote, naye alikuwa akiwapa watu sadaka nyingi, na kumwomba Mungu daima. Akaona katika maono waziwazi, kama saa tisa ya mchana, malaika wa Mungu, akimjia na kumwambia, Kornelio! Akamtazama sana, akaogopa akasema, Kuna nini, Bwana? Akamwambia, Sala zako na sadaka zako zimefika juu na kuwa ukumbusho mbele za Mungu. Sasa basi, peleka watu Yafa, ukamwite Simoni, aitwaye Petro.”

Kwenye sadaka kuna ukumbusho, ndiomaana wachawi kwenye kutoa sadaka zao hawana mchezo, sadaka yako unayotoa ndiyo inayosababisha upokee, chochote apandacho mtu ndicho atakachovuna. Unaweza kusema umeokoka huhitaji madhabahu hapana, Ni lazima uwe na madhabahu unayokula chakula (Neno la Mungu). Biblia inasema ulipo moyo wa mtu ndipo ilipo hazina yake. Kama huna madhabahu maalum unajichelewesha bure, ni lazima ujue madhabahu yako ni ipi na ukishaijua basi utatenda sawasawa na madhabahu hiyo.

Unaweza ukawa umeokoka lakini umeshikiliwa na magonjwa sababu ya madhabahu iliyokushikilia.

Lazaro alivikwa sanda alipokufa lakini Yesu alipomfufua alikuwa bado anazo sanda zake na leso ndipo akaamuru wamfungue aende zake, leo hii kuna watu wameokoka lakini bado wamevalishwa sanda kutokea kwenye madhabahu za ukoo na waganga/

wachawi ili wasiende kwenye hatima zao, watu wengi wameokoka lakini wameungamanishwa kwenye madhabahu za kishetani wao bila kujua na leo hii wanahangaika na mfumo wao wa masisha umeharibika kwasababu ya muunganiko wa madhabahu zilizowashikilia. Sababu zilizofanya washikiliwe ni pamoja na:-

1. KAFARA. Ni sadaka inayotolewa kwenye madhabahu fulani, unapotoa sadaka kwenye madhabahu maana yake umejiungamanisha na madhabahu hiyo wewe na watu wako wote.

Waebrania 9:28 “kadhalika Kristo naye, akiisha kutolewa sadaka mara moja azichukue dhambi za watu wengi; atatokea mara ya pili, pasipo dhambi, kwa hao wamtazamiao kwa wokovu.”

Waebrania 7:1-6 “Kwa maana Melkizedeki huyo, mfalme wa Salemu, kuhani wa Mungu aliye juu, aliyekutana na Ibrahimu alipokuwa akirudi katika kuwapiga hao wafalme, akambariki;amba

ye Ibrahimu alimgawia sehemu ya kumi ya vitu vyote; (tafsiri ya jina lake kwanza ni mfalme wa haki, tena, mfalme wa Salemu, maana yake, mfalme wa amani; hana baba, hana mama, hana wazazi, hana mwanzo wa siku zake, wala mwisho wa uhai wake, bali amefananishwa na Mwana wa Mungu); huyo adumu kuhani milele. Basi, angalieni jinsi mtu huyo alivyokuwa mkuu, ambaye Ibrahimu, baba yetu mkuu, alimpa sehemu ya kumi ya nyara. Na katika wana wa Lawi nao, wale waupatao ukuhani, wana amri kutwaa sehemu ya kumi kwa watu wao, yaani, ndugu zao, kwa agizo la sheria, ijapokuwa wametoka katika viuno vya Ibrahimu. Bali yeye, ambaye uzazi wake haukuhesabiwa kuwa umetoka kwa hao, alitwaa sehemu ya kumi kwa Ibrahimu, akambariki yeye aliye na ile ahadi.”

Ezra 3:3-7 “Wakaiweka madhabahu juu ya msingi wake; maana hofu imewashika kwa sababu ya watu wa nchi; wakamtolea Bwana sadaka za kuteketezwa juu yake, sadaka za kuteketezwa za asubuhi na jioni.Wakaishika Sikukuu ya Vibanda, kama ilivyoandikwa, wakatoa sadaka za kuteketezwa za kila siku kwa hesabu yake, kama ilivyoagizwa, kama ilivyopasa kila siku;na baadaye sadaka ya kuteketezwa ya daima, na za mwandamo wa mwezi, na za sikukuu za Bwana, zilizoamriwa na kuwekwa wakfu, na za kila mtu aliyemtolea Bwana sadaka kwa hiari yake.Tangu siku ya kwanza ya mwezi wa saba walianza kumtolea Bwana sadaka za kuteketezwa, lakini msingi wa hekalu la Bwana ulikuwa haujawekwa bado.”

Kafara inauwezo wa kuungamanisha mtu mfumo wa maisha yake na vizazi vyake, maisha yako namna yalivyo inawezekana ulifungwa kwenye kafara ya madhabahu ya namna Fulani, wayahudi walikuwa wanafanya hivyo kwa Yehova, kwa uhakika maisha ya mtu yanaweza kufugwa kutokana na sadaka au kafara iliyomkamata.

“kwa jina la Yesu naharibu kafara zilizoniungamanisha na madhabahu zilizonishikilia” Amen.

2. Majina uliyopewa yanaweza kukungamanisha na miungu wa madhabahu Fulani.

Usipende kupokea majina ambayo yana maagano au hujui asili yake ni nini yanaweza kuungamanisha na nguvu za giza ukawa unapatwa na matatizo bila wewe kujua.

3. Maagano yanaweza kumuungamanisha mtu na madhabahu inayoweza kuleta matatizo.

Wengine wanatoa maagano ya kucha, vitovu, wanachanja chale kwenye familia zao ili kufanya maagano na miungu bila kujua wanaingiza kwenye matatizo familia zao kwa kujifanya wanalinda watoto wao na mabaya. Ni vizuri unapopata mtoto utafute wachungaji wa kwenye Madhabahu ya Yehova wakiusaidie badala ya kufanyia maagano na miungu ya kichawi.

Mambo ya Walawi 17:10-13 “Kisha mtu awaye yote wa nyumba ya Israeli, au miongoni mwa hao wageni wakaao kati yao, atakayekula damu, ya aina yo yote, nitakunja uso wangu juu ya mtu huyo alaye damu, nami nitamkatilia mbali na watu wake. Kwa kuwa uhai wa mwili u katika hiyo damu; nami nimewapa ninyi hiyo damu juu ya madhabahu, ili kufanya upatanisho kwa ajili ya nafsi zenu; kwani ni hiyo damu ifanyayo upatanisho kwa sababu ya nafsi. Kwa hiyo naliwaambia wana wa Israeli, Hapana mtu miongoni mwenu aliye na ruhusa kula damu, wala mgeni aketiye kati yenu asile damu”

Kafara za Damu ulizozitoa kwa waganga wa kienyeji Bado zinaongea zinaweza kukushikilia na kukupelekesha kwenye umaskini na matatizo mpaka utakapotumia Damu ya Mwanakondoo Yesu Kristo.

Habakuki 3:9-10 “Uta wako ukafanywa wazi kabisa; Viapo walivyopewa kabila vilikuwa neno thabiti; Ukaipasua nchi kwa mito. Milima ilikuona, ikaogopa; Gharika ya maji ikapita; Vilindi vikatoa sauti yake, Vikainua juu mikono yake.”

Amosi 1:6-8 “Haya ndiyo asemayo Bwana; Kwa makosa matatu ya Gaza, naam, kwa manne, sitaizuia adhabu yake isimpate; kwa sababu waliichukua katika hali ya kufungwa kabila nzima, wawatie katika mikono ya Edomu; lakini nitapeleka moto juu ya ukuta wa Gaza, nao utayateketeza majumba yake. Nami nitamkatilia mbali mwenyeji katika Ashdodi; na yeye aishikaye fimbo ya enzi katika Ashkeloni; nami nitaugeuza mkono wangu uwe juu ya Ekroni; na mabaki ya Wafilisti wataangamia, asema Bwana MUNGU.”

Mwanzo 49:3-5 “Reubeni, u mzaliwa wangu wa kwanza, Nguvu zangu, na malimbuko ya uwezo wangu. Umewapita wengine kwa ukuu na kwa nguvu. Umeruka mpaka kama maji, basi usiwe na ukuu, Kwa sababu ulikipanda kitanda cha baba yako, Ukakitia unajisi; alikipandia kitanda changu. Simeoni na Lawi ni ndugu; Panga zao ni silaha za jeuri.”

Ruben alilala na mke wa mzaliwa wa Baba yake, jambo hilo lilikatosha kumwondolewa haki yake ya mzalwia wa kwanza, ikahamishiwa kwa Yusufu watoto wake wakapewa.

1 Mambo ya Nyakati 5:1-3 “Na wana wa Reubeni, mzaliwa wa kwanza wa Israeli; (kwa maana ndiye aliyekuwa mzaliwa wa kwanza, lakini, kwa kuwa alikinajisi kitanda cha babaye, haki yake ya mzaliwa wa kwanza walipewa wana wa Yusufu, mwana wa Israeli; tena nasaba isihesabiwe kwa kuifuata hiyo haki ya mzaliwa wa kwanza. Kwani Yuda ndiye aliyeshinda miongoni mwa nduguze, na kwake ndiko alikotoka mtawala; bali haki ile ya mzaliwa wa kwanza alipewa Yusufu); wana wa Reubeni, mzaliwa wa kwanza wa Israeli; Hanoki, na Palu, na Hesroni, na Karmi.”

4. Kuingia katika eneo ambalo wanaabudu miungu mingine, inatosha kujiungamanisha na madhabahu inayoweza kukuletea matatizo.

Ni vizuri kuangalia sehemu ambayo unaingia kuabudu kama moyoni mwako hauna amani ondoka mahali ili kuepuka kujiungamanisha na madhabahu yenye za kishetani. Kama umeokoka na hujasimama vizuri hujazwa roho mtakatifu vizuri unaweza kukamatwa na madhabahu ambazo sio za Mungu Yehova.

Waamuzi 2:11-14 “Wana wa Israeli walifanya yaliyokuwa ni maovu mbele za macho ya Bwana, nao wakawatumikia Mabaali.Wakamwacha Bwana, Mungu wa baba zao, aliyewaleta kutoka katika nchi ya Misri, wakafuata miungu mingine, baadhi ya miungu ya watu wale waliokaa karibu nao pande zote, wakajiinamisha mbele yao; wakamkasirisha Bwana, akaghadhibika. Wakamwacha Bwana, wakamtumikia Baali na Maashtorethi. Hasira ya Bwana ikawaka juu ya Israeli, naye akawatia katika mikono ya watu waliowateka nyara, akawauza na kuwatia katika mikono ya adui zao pande zote; hata wasiweze tena kusimama mbele ya adui zao.”

5. Kujiingiza kwenye agano la ndoa.

Huu mfumo hugeuza maisha ya mtu na hatima yake na unakua mtu tofauti kabisa, unapoingia kwenye agano la ndoa mfumo wako wa kimaisha unabadilika kabisa. Kuna mtu akioa/olewa alikua anaomba kabla hajaoa/

olewa lakini tangu alipoingia kwenye ndoa hawezi tena kuomba anakua mtu mzembe na mvivu. Mtu mwingine anapoingia kwenye ndoa anakuwa tofauti anaanza kuchangamka na kungaa kwasababu ya madhabahu iliyomuunganisha na mwenza wake imefanya agano lao la ndoa limekua imara. Kabla hujaoa/olewa angalia madhabahu ya mtu unayetaka kuungana naye sababu maisha ya mtu yameungamanishwa na shetani au Mungu Yehova.

Waamuzi 3:4-8 “Naye aliwaacha ili awajaribu Israeli kwa hao, apate kujua kwamba watasikiliza amri za Bwana, alizowaamuru baba zao, kwa mkono wa Musa. Basi wana wa Israeli wakaketi kati ya Wakanaani; hao Wahiti, na hao Waamori, na hao Waperizi, na hao Wahivi na hao Wayebusi; wakawaoa binti zao, na binti zao wenyewe wakawaoza wana wao waume, na kuitumikia miungu yao. Wana wa Israeli walifanya yaliyo maovu mbele za macho ya Bwana, nao wakamsahau Bwana, Mungu wao, nao wakawatumikia Mabaali na Maashtorethi.”

Kitendo cha kuoa au kuolewa kinatosha kuingia kwenye madhabahu nyingine. Ulikua una kazi nzuri, ulipooa tu ukapoteza kazi, ulikua unaamani ulipoolewa huna amani tena, ndoa ni eneo tosha la kubadilisha maisha kuwa mazuri au mabaya.

(Unatakiwa usimame kwa mamlaka ya Jina la Yesu haribu na jitenge na madhabahu zilizokushikilia kwenye maisha yako iwe kutokana na ndoa, maagano ya familia, kafara, sadaka, kuabudu sanamu jitenge na tabia za ukoo na kifamilia kwa damu ya Mwanakondoo, haribu kila ugonjwa wa kurithi, umaskini unaofanana, kutokusoma kama wanaukoo, kuolewa na kuachika kama ndugu zako, kupata na kupoteza kama ndugu zako unatakiwa ukatae kwa damu ya Yesu na kataa jina la ukoo wako kwasababu unaweza ukawa unajiungamanisha na kafara zilizotolewa na mababu zako miaka ya nyuma pamoja na mikataba iliyowekwa ambayo inakushikilia mpaka leo, tamka kwa kinywa chako mwenyewe na utakua huru kwa jina la Yesu, hamia kwenye ukoo wa Ibrahimu, Isaka na Yakobo, ukoo wa Yesu Kristo ambao asili yake ni mamlaka, nguvu na utajiri wa Mungu. Futa jina lako kwenye kitabu cha maagano ya ukoo kwa jina la Yesu