Lolote baya au zuri haliwezi kukupata bila taarifa. Mungu ni Mungu wa taarifa hawezi kukupa kitu au jambo bila hukupa taarifa kwanza.
Amosi 3:7 “Hakika Bwana MUNGU hatafanya neno lo lote, bila kuwafunulia watumishi wake manabii siri yake.”
Kama unamtumaini Mungu afanye jambo lolote kwako fahamu kwanza anaweza kuwafunulia watu wake kabla hawajapata jambo watakalo.Ndoto tunazoota kimsingi zimebeba mambo ambayo hutokea baadae.
MUNGU HUONGEA KWA NAMNA 5.
1. Kupitia Neno lake
Yeremia 1:4 “Neno la Bwana lilinijia, kusema”
2. Kupitia watumishi wake au watu.
3. Pia Mungu anaweza kuongea nasi kupitia maono, maono ni tofauti na ndoto. Ili uone maono lazima macho haya ya nyama yafumbe yafunguke ya rohoni.
4. Anaweza kuongea kupitia mazingira. Jambo la tano Mungu anaonea kupitia ndoto.
Yoeli 2:28-30 “Hata itakuwa, baada ya hayo, ya kwamba nitamimina roho yangu juu ya wote wenye mwili; na wana wenu, waume kwa wake, watatabiri, wazee wenu wataota ndoto, na vijana wenu wataona maono; tena juu ya watumishi wenu, wanaume kwa wanawake, katika siku zile, nitamimina roho yangu. Nami nitaonyesha mambo ya ajabu katika mbingu na katika dunia, damu, na moto, na minara ya moshi.”
Kuna mambo Mungu anaweza kutuonyesha mojawapo mambo yajayo kupitia ndoto. Ndoto zimebeba ujumbe wa leo au kesho au baada ya miaka mitano.
inawezekana kuna matukio yamekupata lakini kama ungalijua mwanzo hayo yasingekupata kama ungetilia maanani ndoto ulizoota na kuzichukulia hatua. Ndoto inaweza kuharibu maisha ya mtu au kuinua maisha ya mtu.
Danieli 2:1-28
Watu wasiomjua Mungu wakiota ndoto mbaya huwa zinawasumbua sana lakini watu wa Mungu mara nyingi hudharau ndoto mbaya na kuona hazitawapata kwasababu wameokoka na ni wana wa Mungu. Ni kweli lakini hio pekee haizuii ni lazima usimame uchukue hatua mwenyewe kwa jina la Yesu.
Mungu anatufunulia mambo mengi kwa njia ya ndoto sababu ya ubize wetu. Watu wapo bize na mambo yao hata Mungu anapoongea nao kwa njia ya ndoto hawachukui hatua na kile walichokiota wanasubiri mpaka wakija kupata matatizo wanaanza kumlilia Mungu na kumtafuta lakini wangeshughulikia ndoto zile mabaya mabaya hayo yasingewapata.
Ndoto inaweza kubeba kuinuliwa au kushushwa chini. Ndoto inaweza kubeba miaka 7 ya njaa na miaka 7 ya shibe.
Ndoto ni fumbo na kwasababu hiyo watu wengi wasipoelewa hawachukulii maanani. Kuna tabia wanadamu wanayo ya kutojisumbua ili kupata jambo fulani hawataki njia ndefu ili wapate wanataka njia ya mkato kama kuwekewa mikono, kutabiriwa, kukanyaga mafuta, kula chumvi n.k. Hawataki kuchimba wenyewe neon la Mung wapate ufumbuzi wa maisha yao.
Mathayo 17:21-22 “Lakini namna hii haitoki ila kwa kusali na kufunga.”
Mungu anataka ili upenye upate nyumba au kiwanja mpaka ufunge na kuomba hataki upate kwa kutabiriwa au kukanyaga mafuta kwasababu hutamtukuza Mungu utasema vinapatikana kwa kutabiriwa na mafuta au chumvi.
Kuna mambo mengi tumeshindwa kuyapata kwababu ya sisi kutaka njia ya mkato. Mungu ni mtu wa vita. Kwenye mambo ya vita Mungu anakua mtu je wewe kwanini hutaki kushindana na falme za giza? Ukitaka maisha ya kawaida usishindane lakini kama unataka mambo zaidi ya wastani fanya vita vya rohoni utayapa. Anza saahivi kesho yako haitakua ya kawaida kuna mambo utayaondoa mpaka watu watashangaa umeyaondoaje, umeyapataje kwa jina la Yesu.
Hesabu 12:6-7 “Kisha akawaambia,Siki
zeni basi maneno yangu;Akiwapo nabii kati yenu,Mimi,Bwana,nitajifunua kwake katika maono,Nitasema naye katika ndoto. Sivyo ilivyo kwa mtumishi wangu, Musa; Yeye ni mwaminifu katika nyumba yangu yote; Kwake nitanena mdomo kwa mdomo, Maana, waziwazi wala si kwa mafumbo; Na umbo la Bwana yeye ataliona. Mbona basi ninyi hamkuogopa Kumnenea mtumishi wangu, huyo Musa?”
Ni uaminifu wako unakupelekea Mungu aongee na wewe. Musa alikua mwaminifu mbele za Mungu na Mungu hakuongea naye kwa ndoto sababu alikua mwaminifu. Maisha yajayo Mungu anaweza kuyafunua katika maono au ndoto.
Ukiota ndoto hiyo ni fumbo unatakiwa utafute mchungaji akufunulie hiyo ndoto.
Matukio yanayokupata yanahusiano na ndoto ulizoota. unaweza kuwa hujaiota wewe lakini kuna mtu ameiitoa mahali juu yako. Ukiomba Mungu anakupa majibu na anakuonyesha madhara yatakayokupata kupitia ndoto.
2 Wafalme 6:8 -15
Kuna watu wa siri wanatengeneza mabaya fulani ili jambo baya likupate. Kuna watu kwenye familia wao likimpata mtu jambo fulani wanajua maana yake ni nini sababu wametengeneza wao au wanauhusiano na wanaoyatengeneza.
Maombi na mahubiri hayasaidii kama mtu anasikia neno na halifanyii kazi. Yapo maneno ya Mungu yameachiliwa yamegusa moyo wako Mungu ameongea na wewe unatakiwa uyafanyie kazi. Neno linaweza kugeuka likawa kazi, ndoa, ajira, safari lakini lina hatua zake mpaka ligeuke. Simama imara kama askari wa Bwana Yesu nawe utafanikiwa kwa jina la Yesu.
Neno la Mungu linaoza, Mungu akija kwako usipompokea anaondoka na kwenda mahali pengine. Maana alikuja kwa walio wake wakamkataa bali waliompokea akawafanya kuwa wana wa Mungu.
Ndoto inaweza kubeba ujumbe ukaletewa inayomhusu mtu mwingine. Kila kinachotokea Mungu alishasema kiwe. Mfano mzuri Yesu alizaliwa sababu Mungu akisema.
Mwanzo 28:12
Yakobo akauta ndoto.
Mwanzo 31:24
Labani alionywa na Mungu juu ya Yakoo kupitia ndoo.
Mwanzo 35:8
Mwanzo 40:2-6
Yusufu aliota ndoto kuhusu mwokaji wa Mfalme na mnyeshaji wa Mfalme na zikawa vilevile kama walivyoota akawatafsiria maana yake.
Watu wengi ama ni kukosa maarifa au uzembe au kupuuza ndoto wanazoota. Ulimwengu wa roho ni ulimwengu mama mambo yanayotokea mwilini huanzia huko. Kuna watu wanatengeneza mambo ya sirini lakini Mungu ametupendelea kuyaona kabla hayajatokea kupitia ndoto.
Ndoto inaelezea hali yako ya rohoni. Ukiota unapigana halafu unapigwa wewe unajikinga tu bila kupiga hata ngumi moja mana yake uwezo wako wa rohoni ni kujilinda sio kuwapiga adui zako. Au unaota unapita mahali kuna kinyesi unajaribu kukwepa maana yake umezungukwa na watu wasiofaa waache au hama sehemu hiyo. Unaweza kupuuzia na hata mtu akikuambia njia zako sio nzuri unakataa sababu umeshayazoea maisha yale.
Kuna taarifa nyingine Mungu anakuambia kupitia mtu. Mtu anaweza kuongea mambo yako kupitia mtu hatakama hajui anakuambia wewe huyo ni Mungu anakuambia.
Ndoto zimebeba ujumbe mzuri ama mbaya, mauti au uzima. Kuna mtu anaota amengatwa na mdudu akapuuzia baadaye mguu wake unakuja kuanza kupatwa matatizo. Mungu anaijua kesho yetu hataki tukurupuke anakuandaa mapema ili ujipange na upite katikati yao kwa jina la Yesu.
Kuna matatizo na magumu yapo mbele yako ya kazi au ndoa au biashara Mungu anakujulisha kabla hayajakujia ili uwe imara na kufanikiwa kuyashinda kwa jina la Yesu. Inawezekana leo hii wewe ni mgonjwa lakini Mungu alishasema na wewe kuna watu hawakupendi uwaepuke wamekurushia mapepo ya magonjwa.
KUNA NDOTO AINA 3
1. Kuna ndoto za kawaida za shughuli nyingi za kazi.
Mhubiri 5:3
2. Kuna ndoto za KiMungu. Sulemani aliota Mungu amemtokea mwenye ndoto akampa Hekima.
3. Kuna ndoto za kishetani ambazo zinakuja kwa kutisha na ukiogola tauari shetani amekushinda.
Ayubu 5:5, 3:25
Usiogope ukijawa hofu kila unachofihofia kitakupata. Lengo la shetani ni kuwatia watu hofu. Mtu anaweza kufungwa na wachawi kupitia ndoto. Unaota unakimbizwa na mjusi. Unaingiliwa kimwili. Unakula nyama au vyakula vya ajabu. Unaota umezama kwenye maji. Unaota umengatwa na ngombe. Unaota unanyonyesha wakati wewe ni binti hujawahi kuolewa bado. Maana yake ni tayari umewekwa mwenye vifungo ukija kuolewa unapatwa na matatizo ya ndoa au huolewi au huzai maana yake tayari umeshaolewa ndotoni.
Vifungo na matatizo mengi vimeanza kwa ndoto. Wachawi wanaweza kutengeneza nyoka wakakutumia akakungata wanaweza kutengeneza mnyama yeyote au ndege wakakutumia ndotoni. Ndoto za nyakati hizi ni tofauti na za kwenye Biblia sababu Mungu anaongea na sisi kupitia ndoto na shetani naye anazuia tusione mambo Mungu anayoongea nasi.
Maombi
“katika jina la Yesu leo ninaharibu kila ndoto mbaya kwa jina la Yesu, Bwana Yesu nisamehe kwa kupuuzia ulipoongea na mimi kupitia ndoto leo ninaamuru kila jambo baya nililofungwa au kutumiwa linipate baadae ninaliharibu kwa damu ya Yesu kristo ninasambaratisha mashetani wote waliotumwa kujiingia kupitia ndotoni kwa jina la Yesu amen