Ili kurudisha roho yake itoke shimoni, Ili atiwe mwanga kwa mwanga wa walio hai. Ayubu 33:30,

 Kwa namna hii inaonesha kuwa hata kama mambo yanaweza kupelekwa shimoni bado yanaweza kurudishwa toka shimoni. Kuna mashimo madogo madogo, na binadamu hawezi kufanya kitu chochote pasipo kupewa na Mungu. Kuna eneo la mtu limebarikiwa na kupitia eneo hilo apate kuingia kwenye hatima yake.Shetani hajawahi kuumba kitu chochote, kazi yake ni kuchukua vitu vya watu walivyopowa na Mungu anawapelekea wachawi, nao wanatumia kana kwamba wametengeneza wenyewe. Kuna amabaye siri yake ni ujasiri, ndani ya moyo wake, wachawi wanaweza kutumia ujasiri wako wanatisha watu. Na walio barikiwa miguu yao, kila anakokwenda anafanikiwa, lakini kama imeibiwa waweza kujikwaa mara kwa mara, na ukaanguka mbele za watu.

Shetani anaweza kugeuka na kuwa kitu chochote. Utajiuliza kwanini mtu akitaka kumloga mtu ahawezi kusema ntaenda London, au Kenya? Hii ni kwa kuwa shetsni amechagua maeneo na huko ameweka madhdbahu yake mfano kama unavyosikis Sumbawanga.