**MUNGU WA MADHABAHU ZA KISHETANI
shetani ndiye mungu wa madhabahu za wachawi, waganga wa kienyeji, wasoma nyota na mawakala wote wa mauti.
2Kor 4:4 “ambao ndani yao mungu wa dunia hii amepofusha fikira zao wasioamini, isiwazukie nuru ya injili ya utukufu wake Kristo aliye sura yake Mungu.”
1Wafalme 16:32 “31 Ikawa, kama ingalikuwa neno dogo tu kuyaendea makosa ya Yeroboamu mwana wa Nebati, akamwoa Yezebeli binti Ethbaali, mfalme wa Wasidoni, akaenda akamtumikia Baali, akamsujudia. 32 Akamjengea Baali madhabahu katika nyumba ya Baali, aliyoijenga huko Samaria.”
*****FANYA MAOMBI YA KUWAANGAMIZA MIUNGU WA MADHABAHU ZA KISHETANI*****
KUHANI WA MADHABAHU
Kuhani wa madhabahu ni mtu mwenye uwezo wa kuleta mambo kutoka ulimwengu wa roho kuingiza katika ulimwengu wa mwili.
Mwanzo 14:18 “Na Melkizedeki mfalme wa Salemu akaleta mkate na divai, naye alikuwa kuhani wa Mungu Aliye juu sana.”
**KUHANI WA MADHABAHU ZA KISHETANI
1 Samweli 5:5 “Kwa hiyo makuhani wa Dagoni, na mtu awaye yote aingiaye nyumbani mwa Dagoni, hawakanyagi kizingiti cha nyumba ya Dagoni huko Ashdodi, hata leo.”
1Wafalme 18:25-26 “25 Eliya akawaambia manabii wa Baali, Jichagulieni ng'ombe mmoja, mkamtengeze kwanza; maana ninyi ndio wengi; mkaliitie jina la mungu wenu, wala msitie moto chini. 26 Wakamtwaa yule ng'ombe waliyepewa, wakamtengeza, wakaliitia jina la Baali tangu asubuhi hata adhuhuri, wakisema, Ee Baali, utusikie. Lakini hapakuwa na sauti, wala aliyejibu. Nao wakaruka-ruka juu ya madhabahu waliyoifanya.”
**** FANYA MAOMBI YA KUWAANGAMIZA MAKUHANI WA MADHABAHU ZA KISHETANI
KAFARA YA MADHABAHU
Madhabahu haiwezi kukamilika kama hakuna kafara kwasababu kila mungu wa madhabahu huhitaji kafara.
Walawi 2:2 “kisha atauleta kwa wana wa Haruni, hao makuhani; naye atatwaa konzi moja katika huo unga mwembamba, na katika mafuta yake, na huo ubani wote; kisha kuhani atauteketeza kuwa ndio ukumbusho wake juu ya madhabahu, ni kafara ya kusongezwa kwa njia ya moto, ya harufu ya kupendeza kwa Bwana;”
Zaburi 40:6 “6 Dhabihu na matoleo hukupendezwa nazo, Masikio yangu umeyazibua, Kafara na sadaka za dhambi hukuzitaka.”
Zaburi 50:8 “Sitakukemea kwa ajili ya dhabihu zako, Na kafara zako ziko mbele zangu daima.” INAENDELEA prt 3 By prophet of God