**KAFARA KWENYE MADHABAHU YA KISHETANI
Zaburi 106:36-38 “36 Wakazitumikia sanamu zao, Nazo zikawa mtego kwao. 37 Naam, walitoa wana wao na binti zao Kuwa dhabihu kwa mashetani. 38 Wakamwaga damu isiyo na hatia, Damu ya wana wao na binti zao, Waliowatoa dhabihu kwa sanamu za Kanaani; Nchi ikatiwa unajisi kwa damu.”
Yeremia 32:35 “Tena walijenga mahali palipoinuka kwa Baali, palipo katika bonde la mwana wa Hinomu, ili kuwapitisha wana wao na binti zao katika moto kwa ajili ya Moleki, jambo nisilowaagiza; wala halikuingia moyoni mwangu kwamba walitende chukizo hilo; wapate kumkosesha Yuda.”
****MAOMBI YA KUANGAMIZA KAFARA ZA MADHABAHU ZA KISHETANI
WASHIRIKA WA MADHABAHU
Washirika wa madhabahu ni watu muhimu sana kwenye madhabahu. Kama vile wewe ulivyo ni mshirika wa kanisa Fulani vivyo hivyo kila madhabahu ya kishetani inayo washirika wake.
Eliya alifahamu umuhimu wa kuwa na washirika. 1Wafalme 19:9-10 “9 Akafika kunako pango, akalala ndani yake. Na tazama, neno la Bwana likamjia, naye akamwambia, Unafanya nini hapa, Eliya? 10 Akasema, Nimeona wivu mwingi kwa ajili ya Bwana Mungu wa majeshi; kwa kuwa wana wa Israeli wameyaacha maagano yako, na kuzivunja madhabahu zako, na kuwaua manabii wako kwa upanga; nami nimesalia, mimi peke yangu; nao wanitafuta roho yangu, waiondoe.”
Mungu anamtoa Eliya hofu
1Wafalme 19:18 “Pamoja na hayo nitajisazia katika Israeli watu elfu saba, kila goti lisilomwinamia Baali, na kila kinywa kisichombusu.”
**WASHIRIKA WA MADHABAHU ZA KISHETANI
Hawa ni watu hatari sana, kwakuwa matatizo yote huanzia kwenye madhabahu za kishetani, wanao peleka jina lako/kazi yako/ndoa yako/elimu yako…… ni washirika wa madhabahu ili lijadiliwe kwa lengo la kuharibu maisha yako.
Washirika wa madhabahu ya kishetani mara zote ni watu wako wa karibu
Waamuzi 16:5 “Nao wakuu wa Wafilisti wakamwendea, wakamwambia, Mbembeleze, upate kujua asili ya nguvu zake nyingi, na jinsi tutakavyoweza kumshinda, tupate kumfunga na kumtesa; nasi tutakupa kila mtu fedha elfu na mia moja.”
Mathayo 10:36 “na adui za mtu ni wale wa nyumbani mwake.” Na Mika 7:5-6 “5 Msimwamini rafiki, msimwekee kiongozi tumaini; ilinde milango ya midomo ya kinywa chako ili mkeo alalaye kifuani mwako asijue habari. 6 Kwa maana mwana humwaibisha babaye, na binti huondoka ashindane na mamaye; na mwanamke aliyeolewa hushindana na mavyaaye; adui za mtu ni watu wa nyumbani mwake mwenyewe.”
*Inaendelea sehemu ya 4 By prophet of God