Utajiuliza kwanini ufundishwe malaika wa kuzimu na sio malaika wa Mungu?Inashangaza sana kuona

malaika kutoka mbinguni anaufunguo na wa kuzimu na akafungua mlango wa kuzimu moshi wa shimoni ukatanda juu ya anga . Abadoni maana yake mharibifu-mharabu. Hivyo kazi yake ni kuharibu ndoa, familia, afya, nchi na kila kitu. Na pia anaharibu makusudi.

Imendikwa;

Mwivi haji ila aibe na kuchinja na kuharibu; mimi nalikuja ili wawe na uzima, kisha wawe nao tele. Yohana 10;10.

Hakuna mtu anayewekuzuia kwenda kwenye safari yangu ya mafanikio uliyopangiwa na BWANA.Nyota ni alama ya malaika,kwa kalenda ya Mungu,Mungu ameweka mitihani ya kukufikisha katika ngazi nyingine.Imeandikwa;

Siri ya zile nyota saba ulizoziona katika mkono wangu wa kuume, na ya vile vinara saba vya dhahabu. Zile nyota saba ni malaika wa yale makanisa saba; na vile vinara saba ni makanisa saba.Ufunuo 1:20

Mungu kila akitaka kukuvusha anaruhusu mitihani ili aone utakavyoikabili. Mitihani ya kulogwa, balaa lakini Mungu ametupa roho mtakatifu atupaye kushinda kwa damu ya Mwanakondoo. Imendikwa;

Nao wakamshinda kwa damu ya Mwana-Kondoo, na kwa neno la ushuhuda wao; ambao hawakupenda maisha yao hata kufa. Ufunuo 12:11

Kabla wana wa Israel hawajaingia nchi ya ahadi, ulikuwepo mto jordani, Mungu anaweza kuondoa kila kitu na aone kama utaendelea kumpenda? Mungu anatengeneza njia katikati ya bahari, Mungu atabaki kuwa Mungu tu hata pasipo mwili utamuona BWANA. Matatizo sio matatizo kila siku, lakini kwa namna unavyoitikia kwenye matatizo waweza kutengeneza matitizo mengine. Hakuna tatizo lakudumu katika kuishi kwako, bali kila tatizo lipo ili kukupigisha hatua ya maisha yako.

Mtu anayesema kuzimu haipo anamatatizo makubwa. Kuzimu ni makao makuu ya shetani hapa duniani, ndiko kiti cha enzi cha shetani kilipo.Imeandikwa;

Kama vile wingu likomavyo na kutoweka, Ni vivyo huyo ashukaye kuzimuni hatazuka tena kabisa Ayubu7:9,

Maana mautini hapana kumbukumbu lako; Katika kuzimu ni nani atakayekushukuru? Zaburi 6:5,

Tuwameze hai kama kuzimu, Na wazima, kama wao washukao shimoni. mithali 1:12

Kuna viumbe wa kiroho wanafanya mambo katika ulimwengu wa roho, unapata matatizo katika ulimwengu wa mwili. Uwezo wako wa kushinda katika ulimwengu waroho, ndio uwezo wako wa kushinda katika ulimwengu wa mwili. Kabla ya aibu ya mwilini, inaanzia aibu ya

rohoni, magonjwa ya mwilini yanaanzia rohoni. Lakini Yesu alikufa ili tupate kuwa huru.Imeandikwa;

Na wana wa watu wale waliokutesa Watakuja kwako na kukuinamia; Nao wote waliokudharau Watajiinamisha hata nyayo za miguu yako; Nao watakuita, Mji wa Bwana, Sayuni wa Mtakatifu wa Israeli. Isaya 60:14

Ezekieli31:15, Amosi 9:2 Yona 2:2, Habakuki 2:5 watumishi wa Mungu hawa katika agano la kale walijua kuwa kuzimu ipo. Na pia katika agano jipa Mungu Yesu Kristo alijua kuwa kuzimu ipo. Imeandikwa;

Mathayo 16:18

Mchawi ni mtu anaweza kuwa mwanaume au mwanamke, anaenda kuzimu na kupokea uchawi na nguvu kutoka kuzimu kilipo kiti cha enzi cha shetani. Mshetani waliotoka kuzimu walikuwa na sura ya wadudu, wanadamu, wanyama, hii ni alama kuwa shetani kwa lengo moja la kuharibu atajitokaza katika sura mabli mbali.|Na silaha ya shetani kubwa ni kujificha usimjue, ili apate kuharibu. Kuna kundi la watu na sio watu wa kawaida na wameelekezwa ili wapate kuharibu maishs yako, lakini Mungu naye amaefungua mbingu apate kuwaokoa watu wake.

Unaweza kumuona mtu anavazi la kondoo, kumbe ni mbwa mwitu, anasura ya kibinadamu lakini kumbe ni waharibifu.

Mawazo ya watu duniani ni kuwa usiyemwabudu Mungu ndo mwenye mafaniko, jambo hili sio kweli. Mungu anasema katika mithali nawapenda wale wanipendao na o wanitafutao kwa bidii wataniona naamu na mali idumuyo ni yao. Mungu akikupa maekupa, lakini shetani akikupa ukikiuka mashsrti yake anakunyanganya. Kuna watu kilia wakianza kiti cha mafanikio wanaharibikiwa maana shsetani yule aharibuye anafanya kazi ya kuharibu kila unachokitengeneza.Imeandikwa;

Ayubu 9:31

Ayubu 33:8

Zaburi 28:31

Mithali 1:12

Isaya 22:42

Inawezekana shetani asikuchukue mzima mzima,

akachukua mikono ya mtu au vipawa, muonekano, upendeleo, navyo viksenda shimoni.